Search This Blog

Thursday, January 16, 2020

Mwakingwe afumua kikosi AFC Arusha

By Bertha Ismail

Arusha. Klabu ya AFC Arusha inayoshiriki Ligi Daraja la Kwanza imetangaza kuwaacha wachezaji 16 katika dirisha dogo la usajili

Akizungumza jana, Ofisa Habari wa AFC Arusha Bahati Msilu alisema wamesajili wachezaji wapya 14 kwa lengo la kuimarisha kikosi hicho.

Alisema wachezaji 16 wameachwa kwa sababu mbalimbali zikiwemo za kushuka viwango na wengine waliomba kuachwa ili wasajiliwe na klabu nyingine.

“Klabu yetu ina uzalendo mchezaji akishindwa kuendana na matakwa au kuomba kuondoka hatuwezi kumlazimisha kubaki maana madhara yake tunayajua,”alisema Bahati.

Wachezaji wapya ni Aliphackshard daudi, Raphael Kalolo, Juma Mohammed, Petro Magaya, Mawazo Juma, Musa Mgandi, Benjamin Dominick, Idd Hussein Mogella, Robert Cornel , Francesco Shinyambala, Salum Ramadhani, James Zamba, Aboubakar Juma na David Mwantobe.

“Wachezaji tuliowaacha Isaya Mwaijibe, Andrew Pastima, Yusuph Abdallah, Hassan Sharifu, Mohammed Athumani, Jeilan Amim, Nasil Kassam, Eliya Ramadhani, Mwinda Mwinda, Joshua Ibrahim, Baraka Ally, Shaibu Salum, Rajab Hamisi, Samson Solomon, Idrissa Mohammed na Mbwana Njeche.

Advertisement

Akizungumza jana, Kocha Ulimboka Mwakingwe alisema wamesajili kutokana na maboresho na hakuna madhara ya kuacha idadi kubwa ya wachezaji.

AFC Arusha inashika nafasi ya tatu katika msimamo wa ligi ikiwa na pointi 19 nyuma ya Geita iliyoweka kibindoni 21 sawa na Gwambina.

Let's block ads! (Why?)

No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...