Search This Blog

Tuesday, January 14, 2020

Mtaalam wa kucheza na Nyoka amefariki baada ya kung’atwa na Nyoka

James Paschal, Mkazi wa Mtaa wa Kilimani Kata ya Nsemulwa Manispaa ya Mpanda mkoani Katavi, ambaye ni mtaalam wa sanaa ya kucheza na Nyoka, amefariki Dunia baada ya kung’atwa na Nyoka, wakati akiwa porini akijaribu kuwakamata kwa ajili ya kazi yake.

Akizungumzia tukio hilo mdogo wa marehemu Jefta Paschal, aliyeambatana naye porini kwa ajili ya mawindo, amesema kuwa walifanikiwa kumkamata Nyoka huyo na wakiwa katika harakati za kumuweka kwenye mfuko wa Sulphate, ndipo marehemu aling'atwa mkononi.       

Baadhi ya majirani wa marehemu wamesema kuwa marehemu alifika nyumbani kwake akiwa katika hali mbaya na kuamuru kupelekwa Hospitali, ghafla hali ilibadilika na kufariki Dunia akiwa anapatiwa matibabu.

Mwenyekiti wa Mtaa wa Kilimani Frolence Mbabule, amekiri kutokea kwa tukio hilo na kuwaasa wananchi kuacha kuchezea wanyama wakali kama nyoka.



No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...