Search This Blog

Wednesday, January 8, 2020

Mrema Amuandikia Barua Rais Magufuli ”Nafanyiwa Hujuma”


Mwenyekiti taifa wa Chama cha Tanzania Labour Party (TLP), Augustine Mrema amesema kuwa ameamua kumuandikia barua Rais Dkt John Magufuli juu ya hujuma ambazo amekuwa akifanyiwa na Chama Cha Mapinduzi (CCM) zenye lengo la kumfuta katika ulingo wa siasa.



Mrema amesema kuwa ameamua kumuandikia barua hiyo Rais Magufuli kwa kuwa yeye ni mtetezi wa wanyonge.

“Kuna hila nafanyiwa na Chama Cha Mapinduzi ili kunifuta kwenye ramani za kisiasa bora nimeamua kusema mapema nisinyamaze, na nimeamuandikia barua Rais kwa kuwa nimekua mhanga wa kuonewa.” – Agustino Mrema – Mwenyekiti TLP

“Nilikuwa ‘Very Powerful’ na Ukiwa na nguvu unadhohofishwa, usione sisi tulikuwa tunapendwa na Watanzania na tunaungwa mkono tumedhohofika, vyama vyetu vimekufa, ukadhani watu hawatutaki, ni mbinu na hila.” – Agustino Mrema – Mwenyekiti TLP




No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...