Mshambuliaji wa timu ya taifa ya DR Congo na klabu ya soka ya TP Mazembe Jackson Muleka, ameibuka kinara katika bara la Afrika kwa mwaka 2019, akifanikiwa kuwa mfungaji bora katika michuano ya kimataifa, huku tuzo hiyo kidunia ikichukuliwa na Cristiano Ronaldo.
Katika msimu uliopita ambao ndio huhesabiwa tuzo ya mwaka husika, Muleka alifunga jumla ya magoli 11 kwenye mashindano ya kimataifa, ambapo matatu yalikuwa kwenye timu ya taifa na mengine 8 yakiwa kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika akiwa na TP Mazembe.
Tuzo hiyo ya mshambuliaji bora wa kimataifa hutolewa na International Federation of Football History and Statistics (IFFHS), ambapo kwa mwaka 2019 Ronaldo amechukua baada ya kufanikiwa kufunga magoli 14 akiwa na timu ya taifa ya Ureno na magoli 7 akiwa na Juventus kwenye Ligi ya Mabingwa Ulaya.
Wachezaji waliomfuatia Ronaldo ni Ali Mabkhout (United Arab Emirates), ambaye ana jumla ya magoli 19 kwenye michuano ya kimataifa pamoja na Harry Kane ambaye ana magoli 19 pia akifunga 12 na England na 7 akiwa na Tottenham kwenye ligi ya Mabingwa.
Ronaldo sasa ametwaa tuzo hiyo mara 5 ndani ya miaka 7 akianza mwaka 2013, 2014, 2016, 2017 na sasa 2019.
Search This Blog
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Punguza kilo tano kwa siku saba
NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...
-
Kiwanja kinauzwa kipo Dodoma Mahungu njia ya kwenda Singida kabala hujafika NALA. Kiwanja ni cha Makazi kinaukubwa wa Sqm 450 ( 15 X...
-
Akionekana kwa mara ya kwanza kwa umma tangu aondoke madarakani, aliyekuwa Rais wa Marekani Donald Trump ameweka wazi uwezekano wa kuwania...

No comments:
Post a Comment