Search This Blog

Wednesday, January 15, 2020

Mayanga afunguka kuitema KMC

By Charity James

MSHAMBULIAJI wa zamani wa KMC aliyetolewa kwa mkopo kwenda Ndanda, Vitalis Mayanga amefunguka kuwa yeye ndiye aliyeomba kuondolewa kikosini hapo kutokana na mambo kutomwendea sawa ndani ya klabu hiyo.

Mayanga alijiunga na KMC msimu uliopita kwa mkataba wa mwaka mmoja ambao unatarajia kumalizika mwishoni mwa msimu na ametolewa Ndanda kwa mkataba wa miezi sita.

Akizungumza na Mwanaspoti, alisema ni uamuzi wake kwenda Ndanda na anaamini huko ndio kutamfanya aweze kurudi kwenye ubora wake kama ilivyokuwa misimu miwili iliyopita ambayo iliwashawishi baadhi ya viongozi wa timu mbalimbali na baadaye kutua KMC.

“Sijavunjiwa mkataba mimi ndiye niliyeomba kutolewa kwa mkopo naweza kusema ni kwasababu nilikuwa sipewi nafasi ya kucheza kikosi cha kwanza, hivyo nimeomba kutoka ili nije kuongeza kiwango kwa muda wa miezi sita ambayo nitakuwa huru kwani nitakuwa nimeshamaliza mkataba na klabu hiyo,” alisema.

“Nimebakiza miezi sita tu na ndiyo niliyopewa kuitumikia Ndanda ni muda mwingi kwangu kama nitapata nafasi moja kwa moja kikosi cha kwanza nitakuwa na nafasi ya kupata timu nyingine ndani na nje ya Tanzania kwani malengo yangu sasa ni kujaribu kucheza soka la kulipwa,” alisema.

Aliongeza anaamini kwenye upambanaji na uwezo alionao, hivyo hataweza kutetereka na kurudishwa nyuma. Akiwa na Ndanda atapambana kuhakikisha anakuwa miongoni mwa wachezaji watakaoifanya timu hiyo ibaki Ligi Kuu msimu ujao.

Advertisement

Let's block ads! (Why?)

No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...