Search This Blog

Tuesday, January 28, 2020

Kumbe Stamina Ndiyo Alianza Kusaliti Tangu zamani


MwanaHipHop Stamina ametueleza kitu ambacho hatukijui kutoka kwake, tangu zamani kuwa hakuwahi kuwa muaminifu kwenye suala zima la mahusiano kwani alishafumaniwa mara 2 na aliyekuwa mpenzi wake.

Akiiambia Planet Bongo ya East Africa Radio, inayoruka kila siku za Jumatatu hadi Ijumaa kuanzia 7:00 mchana mpaka 10:00 jioni, Stamina amesema zamani alikuwa anafanya hivyo bila ya kujua thamani ya mwanamke.

"Mimi nimeshawahi kufumaniwa hapo zamani sijawahi kuwa muaminifu, nilikuwa na mwanamke mmoja ambaye nilimtesa kidogo kwa sababu sikuwa na mipango naye ila kumbe yeye alikuwa yupo serious kwangu, tena nilifumaniwa mara 2 na mwanamke huyohuyo mmoja wakati huo nilikuwa sijatulia, sijui nilikuwa sioni thamani yake" amesema Stamina.

Stamina ni moja ya wasanii ambao walikuwa gumzo wiki kadhaa zilizopita, baada ya kuachia wimbo wake wa asiwaze, ambapo amezungumzia yaliyomtokea kwenye ndoa na alivyosalitiwa na mke wake, hali iliyopelekea kuachana kwao.

No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...