Search This Blog

Wednesday, January 29, 2020

Koulibaly hang'oki hata kwa sululu Napoli

NAPLES, ITALIA . BEKI wa kati kisiki, Kalidou Koulibaly hatahamia Ligi Kuu England ndani ya dirisha hili la usajili wa Januari licha ya kufuatiliwa san na Manchester United.
Beki huyo Msenegali, Koulibaly, 28, alikuwa akifuatiliwa sana na Man United ndani ya mwaka mmoja uliopita sambamba Chelsea waliokuwa wakicheki uwezekano wa kumng'oa kutoka Napoli. Lakini, sasa ataendelea kubaki na klabu yake ya Serie A hadi mwisho wa msimu. Kwenye dirisha lililopita la majira ya kiangazi Man United walipeleka maombi ya kumsajili beki huyo, lakini wakakutana na kigingi kutoka kwa mmiliki wa Napoli, Aurelio De Laurentiis kwamba hakuna tayari kumuuza staa wake huyo. Kutokana na hilo, miamba hiyo ya Old Trafford iliamua kwenda Leicester City kumsajili Harry Maguire, ambaye kwa sasa ndiye nahodha.
Lakini, kwa sasa huko Napoli kumeibuka malumbano baina ya De Laurentiis na wachezaji wake baada ya kuondoka kocha Carlo Ancelotti kitu kilichodaiwa kwamba kingemsukuma Koulibaly kuhamia Old Trafford Januari hii.
Bosi huyo wa Napoli anaonenkana kuwa mgumu sana na Napoli bado wanamthaminisha beki wao huyo kuwa na thamani ya Pauni 100 milioni. Koulibaly bado ana mkataba wa miaka mitatu na nusu katika kikosi hicho baada ya kusaini dili jipya Septemba 2018.

Let's block ads! (Why?)

No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...