Search This Blog

Wednesday, January 22, 2020

Kizazi kipya Madrid ni Pesa ndefu

MADRID, HISPANIA . KIZAZI kipya cha Real Madrid kimeigharimu klabu hiyo Euro 132 milioni kukiandaa hii ni baada ya kukamilisha usajili wa kinda Reinier Jesus, 18, kutoka Flamengo.

Reinier ametua Santiago Bernabeu kwa dau la Euro 30 milioni, kinda huyo anaungana na wachezaji wengine vijana wa kikosi hicho ambao walisajiliwa kwa fedha kubwa ambao wanaandaliwa kuja kuunda kizazi kijacho cha Madrid.

Wachezaji hao ni pamoja na Rodrygo Goes (Euro 50 milioni), Vinicius Junior (Euro 45 milioni), Marco Asensio (Euro 4 milioni), Martin Odegaard (Euro 3 milioni) na Take Kubo (Bure).

Katika miaka ya karibuni Madrid inaonekana kubadili sera zake za usajili kutokana na kutumia Pesa nyingi kusajili makinda wenye vipaji ambapo makinda wote hao hapo juu wastani wa umri wao ni miaka 22 na kwa jumla wameigharimu timu hiyo Euro 132 milioni.

Let's block ads! (Why?)

No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...