Search This Blog

Wednesday, January 15, 2020

Kiungo mpya Azam ataka rekodi

By Thomas Ng'itu

KIUNGO mpya wa Azam FC, Never Tigere amesema ujio wake katika klabu hiyo anatakiwa kuonyesha kuna kiti cha tofauti kati ya mchezaji mzawa na mchezaji anayetoka nje.

Tigere aliyesaini mkataba wa mwaka mmoja na Azam FC, alisema hii ni mara yake ya kwanza kucheza nje ya nchi yake (Zimbabwe), hivyo anataka kuitumia nafasi hii kuonyesha kipaji chake uwanjani na kujitangaza zaidi.

“Sikuwahi kucheza nje ya nchi yangu kwahiyo nafasi hii natakiwa kuitumia vizuri kujitangaza, natakiwa kupambana ndani ya uwanja lakini pia kuweza kuendana na wenzangu,” alisema.

Aliongeza kwa kusema mashabiki wa klabu ya Azam watambue kwamba amekuja kufanya kazi na sio jambo lingine lolote lile.

Ujio wa kiungo huyu unaongeza vita ya namba katika kikosi hicho baada ya awali kuwa na Mudathir Yahya, Frank Domayo na Masoud Abdallah ‘Cabaye’ ambao wanacheza katika nafasi ya kiungo mkabaji.

Kiungo huyu alikuwa katika kikosi cha FC Platinums kilichocheza klabu Bingwa Afrika mwaka huu ana uwezo wa kucheza kama kiungo mkabaji, mchezeshaji na winga wa kulia aliifungia mabao manne klabu yake katika Ligi ya Mabingwa Afrika. Ndani ya kikosi hicho cha Azam, Tigere atakutana na wachezaji wengine wa zamani wa FC Platinums, Dolnlad Ngoma na Obrey Chirwa.

Advertisement

Let's block ads! (Why?)

No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...