
MADRID, HISPANIA . MLIMBWENDE, Katerina Safarova, 21, anatarajia kupima uzito wa penzi lake kwa straika wa Paris Saint-Germain, Neymar Jr, katika kipindi cha televisheni cha Temptation Island.
Katika kipindi hicho ambacho hulenga kupima uzito wa penzi la mtu, huchukuliwa mvulana au msichana aliye katika uhusiano na kuwekwa pamoja na mtu wa jinsi nyingine ili kuangalia kama atachepuka au la.
Ikiwa atafanikiwa kujizuia kuchepuka basi inathibitika anampenda kweli mpenzi wake, lakini akishindwa ni ushahidi kuwa hana penzi la dhati kwa mtu anayetoka naye kwa wakati huo.
Licha ya Neymar kukanusha mara kwa mara Katerina ni rafiki yake wa kawaida tu, lakini watu wa karibu wa wawili hao wanadai ni wapenzi hivyo kitendo cha mrembo huyo kushiriki katika kipindi hicho kinachukuliwa kama kipimo kwa penzi la Neymar.
No comments:
Post a Comment