Msanii Billnass amesema hana lolote la kuongea baada ya kuona picha tata za Nandy akiwa na Ommy Dimpoz ambazo walipiga wakati wanashoot video ya wimbo wao.
Akipiga stori na EATV & EA Radio Digital, kuhusu kuona picha za picha za Nandy Billnass amesema, hayupo sana kwenye maadili ila yupo katika upande wa uandishi, utunzi, hiphop na kufanya show.
"Zile sio picha zangu mimi ajibu mtu mwenye picha zake, sipo sana kwenye maadili nipo kwenye utunzi, uandishi, hiphop na kufanya show suala la maadili kuna baraza wanaweza kuzungumza zaidi, nafanya video kila siku nashoot kwa watu na warembo tofauti na hii ni tasnia ambayo vitu vyote vinavyofanyika navijua" ameeleza Billnass
Aidha Billnass ameachia Comment kwenye picha ya Nandy baada ya kuona picha hizo ambapo ameandika "Haaaa eeeh Mungu tuvushe mpaka mwezi Juni".
Picha za Nandy na Ommy Dimpoz ambazo zimepostiwa katika kurasa zao za mtandao wa kijamii wa Instagram zimezua gumzo mitandaoni kutokana na mapozi na mavazi ya picha hizo.
Search This Blog
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Punguza kilo tano kwa siku saba
NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...
-
Kiwanja kinauzwa kipo Dodoma Mahungu njia ya kwenda Singida kabala hujafika NALA. Kiwanja ni cha Makazi kinaukubwa wa Sqm 450 ( 15 X...
-
Akionekana kwa mara ya kwanza kwa umma tangu aondoke madarakani, aliyekuwa Rais wa Marekani Donald Trump ameweka wazi uwezekano wa kuwania...

No comments:
Post a Comment