Search This Blog

Friday, January 31, 2020

Guardiola akubali mziki wa Maguire

MANCHESTER, ENGLAND . PEP Guardiola amemwaga sifa kwa mastaa watano wa Manchester United ambao wamemkosha sana kwenye mchezo wa marudiano wa nusu fainali ya Kombe la Ligi ambapo waliichapa timu yake ya Manchester City 1-0 uwanjani Etihad.
Hata hivyo, chama la Guardiola ndilo lililotinga fainali kwa kusonga mbele kwa jumla ya mabao 3-2 baada ya mchezo wa kwanza uliofanyika Old Trafford kuibuka na ushindi wa 3-1. Kwenye fainali itakipiga na Aston Villa uwanjani Wembley.
Na Guardiola anaamini timu yake itacheza vizuri kwenye mchezo huo wa fainali utakaopigwa Machi baada ya kucheza chini ya kiwango dhidi ya Man United.
Baada ya filimbi ya mwisho katika mchezo huo, Guardiola aliyataja majina ya wachezaji watano ambao hakika walimfurahisha kutoka kwenye kikosi cha wapinzani wake, ambao ni Victor Lindelof, Luke Shaw, Harry Maguire, Fred na Nemanja Matic.
"Nimependa namna walivyokuwa wakicheza," alisema Guardiola.
"Old Trafford tulicheza vizuri sisi, pengine sikutarajia hivi tulivyocheza, unaweza kusema kwamba hatukuhitaji sana, lakini ukweli ni kwamba wachezaji wao walikuwa vizuri, walicheza kwa namna ile kocha wao alihitaji wacheze.
"Pengine wanashida tu ya kucheza kwa ubora uleule kila mechi, wanashinda wanapocheza nyumbani, lakini ni timu inayocheza soka safi. Namjua Lindelof nilimwona Benfica, Luke Shaw ni mchezaji mzuri na Maguire ni mmoja kati ya mabeki bora kabisa wa kati duniani."

Let's block ads! (Why?)

No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...