Katika yake na alikiba anayejulikana kwa jina la Issa Azam ambaye wamekuwa wote na Alikiba tangu utotoni katika mtaa wa Hombo mkoani Kigoma licha ya yeye kwa sasa kufanyia kazi zake Dar Es Salaam amefungukla mwanzo mwisho kuhusu Alikiba ambao walilelewa nyumba moja kabla ya Alikiba kuja Dar kwa Wazazi wake na kuanza harakati za Maisha.
Akiwa shabiki mkubwa wa Diamond anasema kuwa mwanzo kabisa alikuwa anawashabikia wote lakini tatizo lilianza pale Alikiba na Diamond walipotofautiana na yeyey hakuwa na namna ilibidi afuate moyo wake unatakaje na moyo wake ulikuwa unamkubali sana Diamond kuliko Alikiba hasa yale majigambo ya Diamond na upambanaji wake.
Issa anaongeza kuwa ndugu zake walianza kumtenga baada ya kuona kuwa hamshabikii Alikiba ambaye ni ndugu yake na badala yake yeye anamshabikia Diamond ambaye sio ndugu yake kwa maana nyingine alionekana msalitti ndani ya familia.
Issa aliendelea kuongea na kusema alishawahi kupigwa mara mbili na mashabiki wa Alikiba hadi kuumizwa vibaya na hapo ndipo Diamond aliposikia na kuanza kuwa nae karibu, lakini baadaye sana famililia ilikuja kuona haya ni mambo ya vijana ni kama watu kutoka familia moja kushabikia timu tofautitofauti kama vile ndugu wanaweza kupishana wengine kushabikia Simba na wengine kushabikia Yanga.
Search This Blog
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Punguza kilo tano kwa siku saba
NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...
-
Kiwanja kinauzwa kipo Dodoma Mahungu njia ya kwenda Singida kabala hujafika NALA. Kiwanja ni cha Makazi kinaukubwa wa Sqm 450 ( 15 X...
-
Akionekana kwa mara ya kwanza kwa umma tangu aondoke madarakani, aliyekuwa Rais wa Marekani Donald Trump ameweka wazi uwezekano wa kuwania...

No comments:
Post a Comment