Search This Blog

Thursday, January 30, 2020

Chelsea wamkumbuka Courtois kisa Kipa kimeo

LONDON, ENGLAND. ASIKWAMBIE mtu, Chelsea wanammisi sana kipa wao wa zamani Thibaut Courtois anayefanya mambo yake huko Real Madrid na kuifanya kuwa timu yenye ukuta mgumu zaidi Ulaya kwa sasa.
Huko Stamford Bridge kwa sasa wapo kwenye mikono ya Kepa Arrizabalaga, ambaye amekuwa akifanya hivyo na kukosolewa tu mara kibao ndani ya msimu huu.
Huko Real Madrid, Courtois ameruhusu mabao 10 tu kati ya 13 iliyofungwa timu hiyo kwa msimu huu ikishika usukani wa La Liga, huku mabao yao ya kufungwa yakiwa machache kuliko timu nyingine zote kwenye Ligi Kuu tano bora za Ulaya.
Atletico Madrid, Paris Saint-Germain na Stade Reims zimeruhusu mabao 14, wakati Liverpool na Athletic Bilbao zenyewe zimeruhusu nyavu zao kuguswa mara 15. Inter Milan wanaonekana wagumu kwenye Serie A wamefungwa mabao 18, wakati kwenye Bundesliga, timu iliyofungwa mabao machache ni Borussia Monchengladbach, 21.
Kwa kuwalinganisha makipa Courtois na Kepa, aliyetoka na kuingia Chelsea kunaonekana kuwa na tofauti kubwa sana. Mashabiki wa Chelsea wanajuta kumpoteza kibao wao Courtois kwa kumuuza kwa Pauni 38 milioni tu kwenda Bernabeu, wakati wao walimchukua Kepa kuja kuchukua nafasi yake akitokea Bilbao kwa ada ya Pauni 71.6 milioni.
Ndani ya msimu huu, Kepa amecheza dakika 540 zaidi ya zile alizocheza Courtois, lakini ni mechi tano tu ndizo ambazo hajaruhusu wavu wake kuguswa, wakati mwenzake amecheza mechi 10 bila ya kufungwa. Courtois ameruhusu mabao 10, wakati Kepa ameruhusu 32, huku Courtois ana wastani wa kucheza dakika 162 kwa kila bao huku Kepa akiwa na wastani wa dakika 68. Kwenye suala la kuokoa, Kepa amefanya hivyo mara 41 kwenye ligi, wakati Courtois ameokoa mara 36.
Kocha wa Chelsea, Frank Lampard alisema: "Tutalifanyia kazi hilo. Unajua kwenye soka hata uwezo mzuri kiasi gani kuna wakati mambo yanakwama na kubeba sana lawama."

Let's block ads! (Why?)

No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...