Dar es Salaam. Wakati Simba ikiwa katika maandalizi ya mchezo wa watani wa jadi Jumamosi, Meddie Kagere amesema hakuna beki anayemhofia Yanga.
Kagere aliyefunga mabao tisa katika Ligi Kuu Tanzania Bara, alisema anatambua uwezo wa mabeki bora nchini wakiwemo wa Yanga, lakini hana hofu nao kwa kuwa anajiamini..
“Dabi huwa tofauti na michezo mingine ya kawaida natarajia itakuwa mechi ngumu kwasababu kila timu itataka kushinda, lakini hakuna beki ninayemuogop najiamini naweza kufunga mbele ya beki yeyote,” alisema Kagere.
Kagere alifunga bao la ushindi dhidi ya Yanga katika mchezo wa mwisho ambao Simba iliishinda 1-0 Februari 16, 2019.
Wakati huo huo, nahodha wa timu ya wanawake ya Simba ‘Simba Queens’, Mwanahamisi Omari ‘Gaucho’ alisema Yanga wanatakiwa kuwa makini na mshambuliaji huyo kutokana na ubora wake ndani ya eneo la hatari la wapinzani.
“Kagere ni mtafutaji muda wowote anaweza kuleta madhara. Kwa mtazamo wangu mechi itakuwa ngumu Yanga ina wachezaji wazoefu kama Kelvin Yondani,” alisema Mwanahamisi.
Kagere na Yondani watakuwa kivutio katika mchezo huo kutokana na ubora na uzoefu wao katika mechi kubwa ikiwemo ya watani wa jadi ambayo Simba itakuwa mwenyeji Jumamosi.
Search This Blog
Thursday, January 2, 2020
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Punguza kilo tano kwa siku saba
NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...
-
Kiwanja kinauzwa kipo Dodoma Mahungu njia ya kwenda Singida kabala hujafika NALA. Kiwanja ni cha Makazi kinaukubwa wa Sqm 450 ( 15 X...
-
Akionekana kwa mara ya kwanza kwa umma tangu aondoke madarakani, aliyekuwa Rais wa Marekani Donald Trump ameweka wazi uwezekano wa kuwania...
No comments:
Post a Comment