Muigizaji wa filamu nchini Aunty Ezekiel, amefunguka kuwa anapenda muonekano alionao rafiki yake Wema Sepetu, ila kwa upande wake amesema hana mpango wa kupungua kwa sababu ameridhika na jinsi alivyo.
"Muonekano wake nauona upo poa, hata mimi naona nakaa kwa shida kwa sababu ya ubonge kwa yeye alivyopungua nimependa, ila mimi sina mpango huo kwa kweli nipo poa kwa hivi nilivyo, kama kupungua labda iwe kidogo tu lakini kupungua zaidi sijawahi kuwaza" amesema Aunty Ezekiel.
Aidha Aunty Ezekiel akizungumzia hofu yake ya kupungua amesema,
"Sihofii chochote ila naamini mimi kama tayari ni mama wa mtoto, kwahiyo waswahili wanasema ukiingia leba kuna viungo lazima vibadilike, haviwezi kubaki vile vile na vitu vingine ukivilazimisha inakuwa shida, kwahiyo naukubali huu mwili ukizingatia bado nahitaji kuwa mama zaidi" ameongeza.
Search This Blog
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Punguza kilo tano kwa siku saba
NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...
-
Kiwanja kinauzwa kipo Dodoma Mahungu njia ya kwenda Singida kabala hujafika NALA. Kiwanja ni cha Makazi kinaukubwa wa Sqm 450 ( 15 X...
-
Akionekana kwa mara ya kwanza kwa umma tangu aondoke madarakani, aliyekuwa Rais wa Marekani Donald Trump ameweka wazi uwezekano wa kuwania...

No comments:
Post a Comment