Search This Blog

Thursday, December 12, 2019

Wan-Bissaka shuhuli yake nzito, anakaba aibu

MANCHESTER, ENGLAND . UNAAMBIWA hivi huko kwenye mazoezi ya Manchester United hakuna mchezaji yeyote wa timu hiyo aliyebahatika kupita na mpira mbele ya beki wa kulia, Aaron Wan-Bissaka.
Kiungo wa zamani wa miamba hiyo ya Old Trafford, Darren Fletcher amesema kwamba amekuwa akiwasikia wachezaji wa Man United alipokwenda kwenye mazoezi ya timu hiyo wakimsema Wan-Bissaka jinsi anavyowakaba na kuwafanya wenzake washindwe kabisa kupita upande wake.
Wan-Bissaka alinaswa kwa ada ya Pauni 50 milioni akitokea Crystal Palace kwenye dirisha lililopita na kiwango cha beki huyo wa kulia kwenye kukaba kinawafanya mashabiki wa Man United na hata wachezaji wa timu hiyo kwamba ameshalipa deni la pesa aliosajiliwa.
Fletcher alisema: "Nilizungumza na baadhi ya wachezaji wa Manchester United, walisema kuhusu wanavyopata shida kumpita Wan-Bissaka mazoezini. Amekuwa akiwagomea. Ukweli Wan-Bissaka kuna ufundi kidogo tu, akiwa nao, basi atakuwa beki balaa duniani."
Baada ya kuonyesha kiwango bora kabisa kwenye mechi ya ushindi wa 2-1 dhidi ya Manchester City kwenye Manchester derby, kocha Ole Gunnar Solskjaer alimsifu beki wake huyo wa kulia kwa kile alichomfanya Raheem Sterling, hakupita.
"Aaron alicheza dhidi ya Raheem Sterling, Riyad Mahrez na Kevin De Bruyne na wote hakuna aliyepita," alisema Solskjaer.
Kuhusu kukaba hilo halina tatizo kwa Wan-Bissaka kitu ambacho amebakiza msimu huu ni kufunga na kuasisti.

Let's block ads! (Why?)

No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...