Search This Blog

Sunday, December 8, 2019

VIDEO:House Boy Aiba Hati ya Nyumba na Kwenda Kukopea, Waziri Aagiza RPC Amshughulikie


Mkazi wa Iringa mjini Bi. Lugano Mwadini amejikuta katika deni linalopelekea karibu nyumba yake kupigwa mnada baada kijana wake wa kazi kukopa pesa kiasi cha shilingi 1,000,000 kwa kutumia hati yake ya umiliki wa ardhi ambayo amemuibia.

Kadhia hiyo imetokea wakati wa mkutano wa Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi William Lukuvi kupitia programu yake ya ‘Funguka kwa Waziri’ Mkoani Iringa alipokuwa akisikiliza na kutatua kero za ardhi kwa wananchi wa mkoa wa Iringa katika ukumbi wa Siasa ni Kilimo katika Manispaa ya Iringa.

katika mkutano huo Bi. Lugano alimtuhumu Kijana wake wa kazi kwa kumuibia hati na kuenda kukopa kwa Bw. Laurence Panklas ambaye ni askari wa jeshi la Polisi Mkoani Iringa anayekopesha kwa riba ya 400,000 kila mwezi ambazo kijana huyo hakuweza kuzirudisha kwa wakati jambo lililopelekea kutaka kuuzwa kwa nyumba yake ili kufidia deni hilo.

VIDEO:



No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...