Search This Blog

Saturday, December 7, 2019

Rodgers mshahara juu, awazidi Klopp, Solskjaer

LEICESTER, ENGLAND . BRENDAN Rodgers amesaini dili tamu kabisa huko Leicester City linalomfanya kuwa kocha namba tatu anayelipwa mshahara mkubwa zaidi kwenye Ligi Kuu England.
Kocha huyo alikuwa akihusishwa na kuhamia Arsenal baada ya timu hiyo kumfuta kazi aliyekuwa kocha wao Unai Emery. Lakini, sasa Rodgers ameamua kubaki zake King Power na kusaini dili tamu kinoma.
Dili mpya la Leicester City linamfanya apandishe mshahara wake kutoka Pauni 5 milioni kwa mwaka hadi Pauni 10 milioni kwa mwaka.
Mshahara huo unamfanya Rodgers awe anazidiwa na Pep Guardiola na Jose Mourinho peke yao kwa makocha wanaolipwa pesa ndefu kwenye Ligi Kuu England.
Guardiola ndiye anayelipwa mshahara mkubwa zaidi, Pauni 20 milioni kwa mwaka huko Manchester City hiyo ni kama Pauni 384,000 kwa wiki. Mourinho anashika namba mbili alikipwa Pauni 15 milioni kwa mwaka huko Tottenham Hotspur licha ya kufukuzwa kazi kwenye klabu mbili zilizopita.
Kisha anafuata Rodgers na baada ya hapo wanafuata makocha wengine akiwamo Jurgen Klopp wa Liverpool, anayelipwa Pauni 7.5 milioni kwa mwaka kama anavyolipwa Ole Gunnar Solskjaer huko Manchester United.
Baada ya hapo ni kocha wa West Ham United, Manuel Pellegrini, anayelipwa Pauni 7 milioni, kisha kocha wa Southampton, Ralph Hasenhuttl, anayepokea Pauni 6 milioni kwa mwaka huku Frank Lampard akilipwa Pauni 5.5 milioni kwa mwaka huko Chelsea.

Let's block ads! (Why?)

No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...