
PARIS, UFARANSA . HABARI ndio hiyo. Mabosi wa Paris Saint-Germain kwa sasa wameanza kumtolea macho kocha wa Real Madrid, Zinedine Zidane.
Mabosi wakubwa wa miamba hiyo ya Ufaransa wanaona inatosha kuwa chini ya kocha Thomas Tuchel na sasa wanamtaka kumwondoa na Zidane aje kuchukua mikoba hiyo.
Kwa mujibu wa mchambuzi maarufu wa soka Eduardo Inda, alifichua kwamba jambo hilo lipo wazi kwamba Tuchel hana maisha marefu kwenye kikosi cha PSG ambapo mabosi wa timu hiyo wanachokitaka kwa sasa ni ubingwa wa Ligi ya Mabingwa Ulaya.
Kitu kingine wanachokiamini kwamba kwa kumpata Zidane basi kuwarahishia kwenye mipango yao ya kunasa mastaa wa maana akiwamo Paul Pogba na wakali wengine kwa sababu wanaamini chini ya kocha huyo watakwenda kubeba mataji mengine kuliko ya ubingwa wa ligi.
"PSG walimfuata Zidane kwenye dirisha lililopita la majira ya kiangazi, lakini hawakupata majibu mazuri," alisema Inda.
"PSG wamechoshwa na Tuchel kwa sababu ya usimamizi wake wa mchezaji (Kylian) Mbappe na wanadhani PSG kocha wanayemtaka kwa sasa ni Zidane."
Taarifa za kutoka Madrid zinafichua kwamba Zidane ataonyeshwa mlango wa kutokea mwishoni mwa msimu huu kama Real Madrid itamaliza bila ya taji lolote.
No comments:
Post a Comment