Search This Blog

Friday, December 20, 2019

Pogba awatia hofu wenzake Man United

MANCHESTER, ENGLAND . WACHEZAJI wa Manchester United baadhi ya maofisa wa timu hiyo wanaamini kwamba Paul Pogba ameshamaliza kucheza  mechi zake kwenye kikosi hicho cha Old Trafford.
Pogba, ambaye amekuwa akitaka kuhama tangu kwenye dirisha lililopita la majira ya kiangazi, hajaichezea Man United tangu Septemba 30 kwa sababu ya kusumbuliwa na maumivu ya mguu.
Staa huyo aliyenaswa kwa Pauni 89 milioni alitarajia arudi uwanjani wikiendi hii, lakini alidaiwa kuumia tena na hivyo kuchelewa kurudi kuitumikia timu yake. Jambo hilo linawafanya baadhi ya wachezaji wenzake kwenye timu na maofisa kudhani kwamba pengine hatavaa tena jezi za Man United hadi hapo atakapoondoka licha ya kocha Ole Gunnar Solskjaer kudai kwamba staa wake atarudi uwanjani hivi karibuni.
Kinachoelezwa ni kwamba Pogba atalazimisha kuhama timu hiyo hasa mwezi ujao wakati dirisha la usajili litakapofunguliwa ili kwenda kutimiza ndoto zake za kujiunga na Real Madrid, ambazo hawajakata tamaa katika kufukuzia saini yake.
Taarifa za kutoka Man United zinadai kwamba hawawezi kumruhusu Pogba kuondoka Januari huku kocha Solskjaer akisisitiza kwamba kiungo huyo yupo kwenye mipango yake licha ya kukosekana uwanjani kwa muda mrefu.
Klabu yoyote inayomtaka Pogba basi itapaswa kulipa Pauni 150 milioni, ikiwa ni karibu mara mbili ya pesa ambazo Man United ililipa ilipomnasa kutoka Juventus kumrudisha Old Trafford mwaka 2016.

Let's block ads! (Why?)

No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...