Search This Blog

Friday, December 20, 2019

Pochettino awakataa Madrid, asubiri simu Man City

MANCHESTER, ENGLAND . MAURICIO Pochettino hana mpango wa kwenda Real Madrid — kwa sababu anawasubiri Manchester City kuona kama watampigia simu kutaka huduma yake mwishoni mwa msimu huu.
Miamba hiyo ya Hispania ilidaiwa kuwa na mpango wa kumpa dili Pochettino baada ya kuonekana kuwa wamejiandaa kuachana na Zinedine Zidane. Lakini, kocha huyo wa zamani wa Tottenham Hotspur amekataa ofa hiyo akitaka kuendelea kubaki kwenye Ligi Kuu England. SunSport linatambua kwamba kuna timu mbili tu ndizo anazozitaka Pochettino huko England, Manchester United na mabingwa Man City. Huko Old Trafford nako amepewa kipaumbele na mabosi wa timu hiyo wakitaka kumpa kazi.
Kumekuwa na wasiwasi kwamba Pep Guardiola huenda akaachana na Man City mwishoni mwa msimu licha ya kwamba atakuwa amebakiza mwaka mmoja kwenye mkataba wake. Pochettino anazitazama timu hizo kwa karibu sana huku akijiweka tayari muda wowote kwenda kuchukua mikoba.
Real Madrid wanamtaka Pochettino baada ya Jose Mourinho kuwavuruga kwenda kujiunga na Spurs. Los Blancos wao walikuwa tayari kumpa pesa Mourinho ili asubiri, lakini Mreno huyo aliamua kutimkia zake Spurs kwenda kutamba dili tamu kabisa la Pauni 12 milioni kwa mwaka.

Let's block ads! (Why?)

No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...