Search This Blog

Sunday, December 15, 2019

Mkuu wa shule anaswa akiomba rushwa ya ngono


Taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa nchini (TAKUKURU) mkoani Dodoma imefanikiwa kumkamata mwalimu mkuu wa shule ya sekondari Serengeti iliopo mkoani Mara Baraka Sabi  (41) akiomba rushwa ya ngono kwa Mwanafunzi  wa kike aliyehitimu kidato cha sita Katika shule hivyo mwaka 2016 ili ampatie cheti chake cha kuhitimu.

Mwanafunzi huyo ambaye jina lake linahifadhiwa kutokana na usalama wake alikuwa anahitaji cheti chake kwa ajili ya kwenda kufanya tartibu za kuomba ajira baada chuo kikuu UDSM. 

Hayo yamesemwa na Mkuu wa Takukuru mkoa wa Dodoma Sosthenes Kibwengo wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini hapo kuhusiana na sakata hilo. 

Kibwengo amesema baada ya Binti huyo kuwasiliana na mwalimu mkuu huyo alimtaka waonane jijini Dodoma ambako alikuwa anahudhiria mkutano wa wakuu wa shule jijini hapa. 

Kibwengo amesema Mwanafunzi huyo ambaye hivi sasa ni muhitimu wa chuo kikuu UDSM baada ya kuona Mwalimu huyo amemwambia asubiri cheti atakuja nacho yeye ndipo akaamua kwenda kutoa taarifa Takukuru kuhusiana na rushwa ya ngono. 

"Mwalimu huyo alimwambia mwanafunzi aende Pai hoteli iliopo jijini hapo Ili ampatie cheti hiko na alipofika alimwambia waende katika chumba walichofikia na kumwambia ampe rushwa ya ngono ndio atampa cheti chake, "amesema Kibwengo. 

"Mwanafunzi baada ya kuona hivyo alimwambia Mwalimu Baraka kuwa wafanye tendo hilo kesho kwa sababu siku hiyo hakuwa vizuri, "amesema Kibwengo. 

Amesema siku inayofuata Mwanafunzi huyo alitekeleza sharti la kwenda kujamiana ndipo Takukuru walifanikiwa kumkamata kumkamata mwalimu mkuu huyo na kuhakikisha ili taratibu za kisheria zifuatwe. 

Kibwengo amesema mtuhumiwa huyo ametenda kosa hilo kinyume na sheria kifungu cha 25 cha sheria ya kuzuia na kupambana na rushwa sura ya 329 ya  marejeo 2018.

Aidha Takukuru imeomba wananchi kuendelea kushirikiana na wadau ili kuendeleza kampeni ya vunja ukimya kataa rushwa ya ngono ili kuhamasisha wananchi kutoa taarifa za vitendo vya rushwa ya ngono. 



No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...