Search This Blog

Tuesday, December 17, 2019

Messi ampiga kijembe Hazard kimtindo

WAKATI pambano la El Classico likizidi kupamba moto kabla ya kukutana hapo kesho Jumatano usiku, Nahodha wa Barcelona, Lionel Messi amempiga kijembe winga wa Real Madrid, Eden Hazard kwamba hawezi kufika uwezo wa Christian Ronaldo.

Messi licha ya kwamba amekuwa akishindanishwa na Ronaldo, amesema uwezo wa Hazard na uwezo wa Ronaldo anayeichezea Juventus hivi sasa ni vitu viwili tofauti anavyoviona.

"Hazard anaweza kufikia uwezo wa Ronaldo? hapna kabisa kwasababu  licha ya kwamba ana uwezo na vitu vingi lakini kiukweli yupo tofauti kabisa na Ronaldo,".

Messi aliongeza kwa kusema "Ni ngumu sana kumlinganisha Hazard na Ronaldo aliyeondoka japokuwa Hazard naye ni mahezaji mzuri sana kiukweli,"

Hazard amesajiliwa na Real Madrid kwaajili ya kuziba pengo la Ronaldo lakini mpaka hivi sasa bado hajaonyesha kile ambacho walikitarajia.

Let's block ads! (Why?)

No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...