Search This Blog

Monday, December 23, 2019

Man United yawaweka sokoni Matic, Rojo

London, England. Manchester United inajiandaa kuwatupia virago Nemanja Matic na Marcos Rojo katika usajili wa dirisha la usajili mwezi ujao.

Kocha Ole Gunnar Solskjaer  amewaweka sokoni Matic na Rojo ili kupata nafasi ya kuongeza wachezaji wapya.

Solskjaer ametoa kauli hiyo akiwa katika maumivu baada ya Man United kufungwa mabao 2-0 dhidi ya timu inayoshika mkia katika Ligi Kuu England Watford.

Man United imekubali kutoa Pauni76 milioni za usajili wa mshambuliaji kinda wa RB Salzburg Erling Haaland.

Klabu hiyo inasubiri ofa ya klabu zinazotaka huduma ya wachezaji ambao kila mmoja amecheza mechi tatu msimu huu.

Matic alipoteza namba kikosi cha kwanza baada ya kupata majeraha ya muda mrefu ingawa Solskjaer alikuwa na mapenzi naye. Mkataba wa mchezaji huyo unamalizika mwishoni mwa msimu huu.

Advertisement

Pia Rojo amekuwa akiandamwa na majeraha Old Trafford na amekuwa mchezaji tegemeo wa timu ya taifa ya Argentina katika nafasi ya beki wa kati na kushoto.

Let's block ads! (Why?)

No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...