
LONDON, ENGLAND. KOCHA wa kipindi cha mpito kwenye kikosi cha Arsenal, Freddie Ljungberg ameitaka bodi ya timu hiyo kumwongezea watu kwenye benchi lake la ufundi ili kurahisha utendaji kazi.
Ljungberg anaona kuwa shughuli imekuwa nzito kutokana na benchi lake kuwa na watu wachache ambapo kwa sasa hivi amekuwa akisaidiwa kwa karibu na Per Mertesacker, ambaye ni kocha wa akademia. Kocha huyo wa muda alisema kwamba Unai Emery alikuwa nan watu wengi kwennye benchi lake kabla ya kufukuzwa mwezi uliopita, hivyo naye angependa kuwa na watu wengi kidogo kufanya mambo kuwa mepesi.
“Ukiona watu waliokuwa kwenye benchi la ufundi hapo kabla, walikuwa wengi sana,” alisema Ljungberg.
“Mimi sina wasaidizi wengi. Kama tutaendelea kuwa hivi kwa miezi kadhaa, basi mambo yatakuwa magumu zaidi. Lakini, hilo ni la klabu wamesema nisubiri hadi watakapofanya uamuzi, hivyo siwezi kufanya chochote. Ninaye Per Mertesacker, lakini yeye ni meneja kwenye akademia, yupo tu hapa ananisaidia kufundisha.”
Tangu alipochukua mikoba ya kuinoa Arsenal, Ljungberg amepata ushindi mara moja kwenye mechi nne, wakati alipowachapa West Ham United 3-1 kwenye Ligi Kuu England. Lakini, beki yake ya kwanza ilikuwa ya kipigo kutoka kwa Brighton kwenye ligi uwanjani Emerates, lakini alipata sare pia ya 2-2 mara mbili dhidi ya Norwich City kwenye ligi na Standard Liege kwenye Europa League.
Leo Jumapili anakabiwa na mtihani mzito kuwakabili Manchester City kwenye mchezo wa Ligi Kuu England utakaopigwa Emirates, huku kiti chake hicho kikihusishwa na makocha kibao akiwamo Carlo Ancelotti, Mikel Arteta na Patrick Vieira.
No comments:
Post a Comment