Search This Blog

Monday, December 16, 2019

Lango ya uchumi lipo Ziwa Tanganyika - TPA


Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA), imesema kuwa lango la uchumi nchini lipo Ziwa Tanganyika kutokana na ziwa hilo kupakana na nchi tatu zenye tapo la utajiri Afrika.

Kutokana na hali hiyo imesema kuwa thamani ya madini yaliyopo Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) unaofikia dola za Marekani trilioni 24, zinahitaji usafirishaji wa uhakika kufika katika soko la dunia.

Meneja wa Bandari za Ziwa Tanganyika, Percival Salama ametoa kauli hiyo mjini Kigoma alipokua akizungumza na waandishi wa habari waliopo kwenye ziara ya kutembelea miradi inayotekelezwa na TPA katika maziwa makuu nchini.

Amesema Bandari za Ziwa Tanganyika zipo katika mikoa mitatu ya Kigoma, Katavi na Rukwa kwa upande wa Tanzania ambapo pia ziwa hilo limepakana na nchi nne kwa pamoja ambazo ni Tanzania yenyewe, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Zambia pamoja na Burundi.

“Na kama unatafuta asilimia ya kila nchi kwenye Ziwa Tanganyika Tanzania ina asilimia 45, DRC 41, Burundi asilimia 8 na Zambia asilimia 6. Na Ziwa Tanganyika ndilo Ziwa la pili kwa kina kirefu duniani lina wastani wa urefu wa kina cha mita 1470, kwa hiyo ukizungumzia uimara wa Biashara ya kuhudumia nchi hizi nne maana yake unazungumzia miaka mingi ijayo.

“Lakini la pili ambalo nataka niliguse kwenye hili eneo ni kwamba Ziwa Tanganyika na mikoa inayopakana na Ziwa Tanganyika na nchi hizi tumelala kwenye utajiri wa kutupwa yaani tupo sisi Tanzania kwenye ukanda wenye utajiri wa kutupwa duniani sio tu katika Afrika.

No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...