
LONDON, ENGLAND. KOCHA wa Chelsea, Frank Lampard amempiga kijembe Jose Mourinho akiponda uamuzi wake wa kuwaacha masupastaa Kevin De Bruyne na Mohamed Salah waondoke Stamford Bridge.
Mourinho, ambaye kwa sasa ni kocha wa Tottenham Hotspur alifanya kazi na mastaa hao wawili katika kipindi chake cha pili alichokuwa kwenye kikosi cha Chelsea. Lakini, wachezaji wote hao walionekana kuwa hawajui na kuondoshwa kwenye timu.
De Bruyne aliuzwa kwenda Wolfsburg kwa ada ya Pauni 18 milioni mwaka 2014 na Salah alienda AS Roma mwaka 2016 kwa ada ya Pauni 12 milioni.
Baadaye wakarudi kwenye Ligi Kuu England, KDB akitua Manchester City na Mo Salah akisaini Liverpool, ambapo kwa sasa wamekuwa mastaa wakubwa sana kwenye timu hizo na kutamba huku Chelsea wakiishia tu kukodoa macho.
Lampard, ambaye Jumapili iliyopita alimchapa kocha wake huyo wa zamani, Mourinho 2-0 timu zao zilipokutana kwenye mchezo wa Ligi Kuu England, alimpiga kijembe Mreno huyo akisema: "Kama ungekuwa makini na kujali mambo yako basi tungekuwa na timu ya wachezaji wazuri na kuendelea kutamba hadi sasa. Klabu ilipoamua kuwauza wachezaji hao, sikuwa mimi kwenye benchi."
No comments:
Post a Comment