
LIVERPOOL, ENGLAND. KOCHA, Jurgen Klopp amesema moja ya sababu zilizomfanya asaini dili la muda mrefu la kubaki Liverpool ni wachezaji wapya wanaopangwa kusajiliwa na miamba hiyo ya Anfield.
Klopp juzi Ijumaa alisaini mkataba mpya utakaomfanya abaki Anfield hadi 2024 huku akiboresha mshahara wake na sasa atakuwa akilipwa Pauni 15 milioni kwa mwaka.
Mjerumani huyo amesema kwamba amekuwa akihusika kwenye mazungumzo ya wachezaji wengi wanaokuja kwenye timu hiyo na hilo ndilo lililomfanya asifikirie kuachana na miamba hiyo, huku kukiwa na ofa kibao klabu nyingine zikimtaka akapige kazi.
“Timu imekuwa ilitaka hili siku nyingi kuhusu suala la kuongeza mkataba," alisema Klopp.
“Lakini, kubwa ni la wachezaji wanaotaka kuja, kwa sababu amekuwa wakiuliza 'ni muda gani kocha ataendelea kuwapo?'. Ndio maana imekuwa hivyo na mambo mengine kama hayo.”
Liverpool wamekwua kwenye kiwango bora kabisa kwa sasa wakitamba kwenye Ligi Kuu England huku dili jipya la Klopp likienda sambamba na usajili wa staa mpya, kiungo Takumi Minamino, aliyenaswa kutooka RB Salzburg kwa ada ya Pauni 7.25 milioni na kwamba atatua rasmi huko Anfield mwezi ujao. Kiraka pia wa timu hiyo, James Milner amesaini mkataba mpya wa kubaki kwennye timu hadi 2022.
No comments:
Post a Comment