Search This Blog

Sunday, December 8, 2019

Januari ngumu kinoma kwa Arsenal

London, England.WANASEMA maisha ya Januari ni magumu, lakini kwa mashabiki wa Arsenal hali itakuwa ngumu zaidi.
Ndio, inakwenda kuwa ngumu kwa sababu Arsenal wanaweza kuingia Mwaka Mpya wakiwa kwenye orodha ya timu zinazopambana zisishuke daraja kama isiposhtuka mapema na kubadili mambo yake haraka.
Kipigo cha nyumbani kutoka kwa Brighton kimewafanya washuke hadi kwenye nafasi ya 10 pointi chache sana juu ya timu zilizopo kwenye hatari ya kushuka. Pointi tano. Lakini, hiyo ilikuwa kabla ya mechi za jana Jumapili, ambapo timu kadhaa zilizokuwa chini ya Arsenal kama Aston Villa, Newcastle United, Southampton, Norwich City na Brighton zote zilikuwa na mechi na pengo la pointi sio kubwa. Baada ya mechi hizo, basi bila ya shaka, msimamo utakuwa umebadilika na Arsenal wanaosubiri kucheza na West Ham United usiku wa leo Jumatatu, pengine hawatakuwa wamebaki kwenye nafasi hiyo ya 10.
Arsenal haijaonja ushindi kwa muda mrefu sana, walitoa sare hadi na timu zinazopambana zisishuke Norwich na Southampton. Kwa mwendo huo na sasa wakiwa hawana kocha wa kudumu, kuna dalili mbaya kabisa zinazoonyesha kwamba, Arsenal watakuwa kwenye wakati mgumu na pengine wataingia Mwaka Mpya 2020 wakichuana wasishuke daraja. Shida ni mechi zinazowakabili ndani ya mwezi huu.
Kwanza kwa kuanzia leo watakabiliwa na mechi ya ugenini kwa West Ham United, ambao wanapambana kuokoa kibarua cha kocha Manuel Pellegrini, huku wakiwa na mzuka wa kutoka kuwafunga Chelsea wikiendi iliyopita. Baada ya hapo watakuwa na mechi dhidi ya mabingwa watetezi ambao wametoka kujeruhiwa, Manchester City.
Kisha watakuwa na mechi nne ndani ya siku 12, wakianzia ugenini kwa Everton. Boxing Day watakwenda kumennyana na Bournemouth kwao na baada ya hapo zitafuata mechi mbili dhidi ya Chelsea na Manchester United. Arsenal watakuwa wameshuka hadi kwenye orodha ya timu tatu za mwisho kama hawatakuwa wameshinda mechi yoyote kati ya hizo huku timu zilizopo chini yake kwa sasa kama zitaendelea kuvuna pointi.
Newcastle United wanaonekana kurudi kwenye kiwango chao, wakati Brighton wameanza kujiamini tangu waliposhinda Emirates. Halafu Burnley watakuwa na mechi zinazoshindika dhidi ya Bournemouth na Aston Villa, wakati Southampton mechi zao tatu zijazo watacheza na timu zilizopo katikati kwenye msimamo wa ligi hiyo. Kama Everton wataishusha Arsenal kama watashinda mechi yao ya Boxing Day dhidi ya Burnley.
Hofu ya Arsenal kuwa kwenye majanga ya kupambana kutoshuka daraja imeanza kumwingia hadi shabiki mnazi wa timu hiyo, Piers Morgan akiandika kwenye ukurasa wake wa Twitter: “Kiwango cha Arsenal kipo hovyo, napata shaka ya kuingia kwenye vita ya kuwania kutoshuka daraja.
“Kama tutaendelea kucheza kwa kiwango kile dhidhi ya Brighton, sipati picha udhalilishaji tutakaokutana kutoka kwa Man City Jumapili. Mtuombee jamani.”

Let's block ads! (Why?)

No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...