Search This Blog

Thursday, December 12, 2019

Emery mpango wake kurudi England

LONDON, ENGLAND . ALIYEKUWA kocha wa Arsenal, Unai Emery anataka kurudi kwenye Ligi Kuu England, lakini kaonekani kama atapata kazi Everton.
Emery hana kazi kwa sasa baada ya kufutwa kazi na Arsenal mwezi uliopita baada ya timu kufanya hivyo ikishindwa kupata ushindi kwenye mechi saba mfululizo.
Kulikuwa na habari kwamba kocha huyo alikuwa kwenye mazungumzo na Everton kwa ajili ya kwenda kuchukua mikoba ya kuinoa timu hiyo yenye maskani yake Goodison Park.
Lakini, ESPN inaripoti kwamba hakuna ofa rasmi ilitolewa na Everton kwa Emery na wanaonekana kuhamishia mipango yao kwa timu nyingine. Emery anataka kurudi kazini haraka iwezekanavyo kuliko kukaa likizo na tayari ameripotiwa kuwa na ofa kibao mezani.
Everton itaendelea kuwa chini ya kocha wa muda, Duncan Ferguson hadi kwenye mechi yao ya Jumapili watakapomenyana na Manchester United. Ferguson aliongoza Toffees kushinda 3-1 dhidi ya Chelsea wikiendi iliyopita baada ya kutua hapo kupewa mikoba ya Marco Silva, aliyefutwa kazi baada ya kuchapwa 5-2 na mahasimu wao Liverpool kwenye Merseyside derby.
Kocha wa zamani wa timu hiyo, David Moyes naye amekuwa akihusishwa na mpango wa kurudi Goodison Park sambamba na Carlo Ancelotti, ambaye hivi karibuni aliachana na Napoli.

Let's block ads! (Why?)

No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...