
LONDON, ENGLAND. KOCHA, Unai Emery amekutana na wasaidizi wake kujadili mpango wa kurudi mzigoni huku ikiripotiwa kwamba amegomea kazi ya kwenda kuinoa Everton baada ya kumfuta kazi Marco Silva.
Emery mwenyewe naye alifunguliwa mlango wa kutokea huko Arsenal, Novemba 29 na tangu wakati huo hana kazi licha ya kuhusishwa na vibarua kibao vinavyomfanya aanze kuwakusanya wasaidizi wake kuona kitu gani wafanye. Kumeelezwa kwamba kuna ofa ya kutoka China kitu ambacho anafikiria ni kwenda kufanya kazi huko kama hatakuwa amebadili mawazo yake kuhusu Everton.
Mambo mengi yamemchomoa Emery kwenye kiti chake huko Arsenal, lakini kubwa ni kushindwa kuipatia timu matokeo mazuri.
Freddie Ljungberg alikuwa msaidizi wake Emery, lakini alipoondoka kwenye timu hiyo mwenzake amebaki na kufanya kuwa kocha wa mpito, akionndoka na wasaidizi wake wengine, Juan Carlos Carcedo na Pablo Villanueva, ambaye alikuwa kocha wa kikosi cha kwanza.
Wawili hao ni marafiki zake wakubwa walicheza pamoja Leganes msimu wa 2002-03 na kwa muda mrefu wamekuwa wakifanya kazi pamoja. Carcedo aliungana na Emery kama msaidizi wake huko Almeria mwaka 2006 na baada ya hapo wamekuwa wakienda pamoja katika kila kazi anayopata huku Villanueva alijiunga kwenye benchi la ufundi la Emery mwaka 2014 alipokuwa Sevilla.
Kocha Emery amekutana na wasaidizi wake kujadili mpango wa kurudi kwenye kazi huku wakihusishwa na kibarua hicho cha Everton baada ya kocha wa Shanghai SIPG, Vitor Pereira kujitoa kwenye mchakato. Lakini, David Moyes, Carlo Ancelotti na Mikel Arteta bado wanaifukuzia kazi hiyo ya Goodison Park.
No comments:
Post a Comment