Search This Blog

Monday, December 9, 2019

Edward Lowassa Ampigia Chapuo JPM Kuongoza Miaka 10 "Tanzania Itapiga Hatua Kubwa Kimaendeleo"


Waziri mkuu za zamani, Edward Lowassa amesema Rais Magufuli akiongoza nchi kwa miaka 10 itapiga hatua kubwa katika maendeleo.

Lowassa  ametoa kauli hiyo katika maadhimisho ya miaka 58 ya Uhuru wa Tanganyika yaliyofanyika mjini Mwanza katika uwanja wa CCM Kirumba.

"Amani ndio msingi anaoutumia mheshimiwa Magufuli leo kuongoza nchi yetu, kuleta mshikamano na umoja, nampongeza amefanya kazi nzuri sana…kama akiachiwa akapiga miaka yake kumi…kumi mheshimiwa nchi hii itabadilika,” – Amesema Lowassa

Lowassa alikihama Chama Cha Mapinduzi (CCM)  mwaka 2015 na kujiunga na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) ambako alipitishwa kugombea urais mwaka 2015 na kushika nafasi ya pili nyuma ya Rais Magufuli katika uchaguzi mkuu, lakini baadaye Machi Mosi, 2019, alirejea CCM.

No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...