NAPLES, ITALIA . ARSENAL na Everton zinatajwa kumtaka Carlo Ancelotti, lakini mpango huo unaweza kuwagharimu pesa nyingi baada ya klabu hizo zote za Ligi Kuu England kusaka makocha wapya kwa sasa.
Klabu hizo mbili zinahusishwa na kocha huyo wa zamani wa Chelsea, Ancelotti baada ya kuachana na Napoli katikati ya wiki.
Mtaliano huyo anatajwa kuwa nafasi kubwa ya kutua huko Arsenal kwenda kuchukua mikoba ya Unai Emery licha ya kudaiwa kwamba kuna orodha ya makocha wasiopungua 10 wanaohusishwa na klabu hiyo ya Emirates. Everton nao wanamtaka baada ya kumfuta kazi Marco Silva wiki iliyopita.
Lakini, taarifa zinadai kwamba Ancelotti anaweza kuwagharimu pesa nyingi timu hizo za fidia kama atakuwa amepewa likizo tu na Napoli, si kwamba amefukuzwa. Kama atakuwa amefukuzwa basi halitakuwa tatizo, Everton na Arsenal zitaweza kumpata bure kabisa, lakini kama atakuwa amepewa mapumziko tu huku akiendelea kupokea mshahara wa Napoli, basi hapo kutakuwa na fidia ndefu.
Kinachoelezwa ni kwamba Ancelotti bado yupo kwenye mambo ya kumalizia kuhusu kuachana na Napoli na hapo atafahamu kama ameachwa jumla au bado anabaki kwenye ratiba ya mishahara ya Napoli hadi mkataba wake utakapofika tamati.
Napoli ilifanya hivyo ilipoachana na Maurizio Sarri kipindi ambacho ilimchukua Ancelotti. Napoli kwa sasa itakuwa chini ya mchezaji wa zamani wa Ancelotti, Gennaro Gattuso, aliyewahi kumnoa huko AC Milan.
Search This Blog
Thursday, December 12, 2019
Dili la Ancelotti utata mtupu
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Punguza kilo tano kwa siku saba
NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...
-
Kiwanja kinauzwa kipo Dodoma Mahungu njia ya kwenda Singida kabala hujafika NALA. Kiwanja ni cha Makazi kinaukubwa wa Sqm 450 ( 15 X...
-
Akionekana kwa mara ya kwanza kwa umma tangu aondoke madarakani, aliyekuwa Rais wa Marekani Donald Trump ameweka wazi uwezekano wa kuwania...
No comments:
Post a Comment