
LONDON, ENGLAND . CHELSEA wameruhusiwa kufanya usajili kwenye dirisha la Januari baada ya mahakama ya michezo kufutilia mbali adhabu yao ya katazo la kusajili.
Fifa iliipiga marufuku Chelsea ya kufanya usajili ndani ya madirisha mawili Februari mwaka jana, hiyo kwa maana dirisha lililopita la majira ya kiangazi na lijalo la majira ya baridi, Januari kitu ambacho wamekata rufaa na kushinda.
Hivyo sasa, Chelsea ina ruhusu ya kusajili jambo litakalomfanya kocha Frank Lampard kuingia sokoni kwenye dirisha la Januari kunasa wachezaji anaowahitaji kuja kuboresha kikosi chake.
Kutokana na zuio la kusajili, kocha Lampard hakuwa na namna zaidi ya kuweka imani kwa makinda Tammy Abraham, Mason Mount, Fikayo Tomori na Reece James, ambao wamekuwa watumishi wa kutegemewa kwenye kikosi hicho cha Stamford Bridge msimu huu, lakini sasa atanasa mastaa anaowataka akiwamo Ben Chilwell wa Leicester City, Alex Telles wa FC Porto, Nicolas Tagliafico wa Ajax na Jadon Sancho wa Borussia Dortmund.
No comments:
Post a Comment