
Saa chache baada ya kushinda rufaa kuzuiwa kusajili kutoka katika mahakama ya (Court of Arbitration for Sport),Chelsea inajipanga kufanya usajili wa kwanza wa watu wanne.
Mmiliki wa klabu hiyo Mrusi Roman Abramovich anaweza kumwaga pesa ili kuongeza wachezaji nyota na taarifa kutoka mtandao wa (The Sun), unaeleza mpaka sasa kikosi hiko cha Chelsea kimeingia vitani kuwanasa wachezaji wanne kutoka katika timu mbalimbali.
Wachezaji hao ni staa wa Borussia Dortmund, Jadon Sancho ambaye amekuwa pia akiwaniwa na timu nyingine kubwa duniani kama Manchester United, Man City na nyinginezo.
Wengine ni beki wa kushoto wa Leicester City, Ben Chilwell ambaye anatazamwa kama kuja kuwa mbadala wa Marcos Alonso, ambaye ameonekana kutokuwa na kiwango kizuri msimu huu.
Mshambuliaji wa RB Leipzig, Timo Werner ni miongoni mwa nyota ambao wanaonekana kuwa chaguo la kocha wa Chelsea Frank Lampard kama ilivyokuwa kwa mshambuliaji wa Bournemouth Callum Wilson.
Hatua hiyo inatokana na Chelsea kufanikiwa kushinda rufaa yake ya kufungiwa katika madirisha mawili ya usajili ambapo sasa wanaweza kuanza kusajili nyota ambao watawahitaji ili kuongeza nguvu katika kikosi chao kuanzia mwezi Januari mwakani katika dirisha la usajili.
No comments:
Post a Comment