Search This Blog
Wednesday, December 4, 2019
CHADEMA Wafunguka Baada Ya Sumaye Kutangaza Kukihama Chama Hicho
Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimesema kuwa kimeshtushwa na kauli za mwanachama wake ambaye ni Waziri Mkuu Mstaafu, Frederick Sumaye aliyetangaza kukihama chama hicho.
Katika mkutano wake na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam uliofanyika leo, Sumaye ametangaza kujitoa Chadema huku akitoa tuhuma mbalimbali kwa mwenyekiti wa chama hicho, Freeman Mbowe.
Mkurugenzi wa Itifaki, Mawasiliano na Mambo ya Nje wa CHADEMA, John Mrema amesema kuwa chama hicho hakikuwa na taarifa za mkutano huo uliofanyika leo na kwamba wameona barua tu mitandaoni kama ilivyokuwa kwa wananchi wengine.
Mrema amesema wamezipokea taarifa za Sumaye kuondoka Chadema na kama mwanachama yoyote ameacha pengo kwenye chama hicho, kwamba watatafuta namna ya kuziba pengo hilo.
“Hatuna taarifa za makundi kwenye chama chetu l kama anavyodai Sumaye, labda kama yeye alikuwa na kundi. Sumaye alikuwa mjumbe wa kamati kuu ya chama alikuwa na nafasi ya kutoa taarifa hiyo na kama kweli ipo ingefanyiwa kazi.
Kuhusu uchaguzi wa chama hicho unaoendelea, Mrema amesema katiba ya Chadema hairuhusu mgombea kupita bila kupingwa, kama mgomba ni mmoja lazima apigiwe kura ya ndio au hapana.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Punguza kilo tano kwa siku saba
NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...
-
Kiwanja kinauzwa kipo Dodoma Mahungu njia ya kwenda Singida kabala hujafika NALA. Kiwanja ni cha Makazi kinaukubwa wa Sqm 450 ( 15 X...
-
Akionekana kwa mara ya kwanza kwa umma tangu aondoke madarakani, aliyekuwa Rais wa Marekani Donald Trump ameweka wazi uwezekano wa kuwania...
No comments:
Post a Comment