Search This Blog

Saturday, December 7, 2019

CHADEMA Kushiriki maadhimisho ya miaka 58 ya Uhuru Jijini Mwanza

Kamati kuu Chadema imeazimia kushiriki maadhimisho ya miaka 58 ya Uhuru wa Tanganyika.

Hii itakuwa ni mara ya kwanza kwa chama hicho kushiriki maadhimisho hayo yanayofanyika kila Desemba 9 tangu kumalizika kwa uchaguzi mkuu mwaka 2015.

Taarifa iliyotolewa na Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano wa Chadema, Tumain Makene imesema hatua hiyo inalenga kukuza na kuendeleza uraia mwema, uzalendo na mapenzi ya nchi yetu.

“Kamati kuu ya Chadema imeazimia kwa kauli moja kuwa Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe aongoze ujumbe wa baadhi ya viongozi wakuu na waandamizi wa chama watakaokiwakilisha chama kushiriki katika maadhimisho hayo.”

“Chama kinawaelekeza wanachama na wapenzi wake jijini Mwanza na maeneo ya jirani kujumuika na Watanzania wengine kushiriki na kuadhimisha siku hii muhimu kwa Taifa letu,” amesema Makene


No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...