Search This Blog

Wednesday, December 18, 2019

BREAKING: Mbowe ashinda uchaguzi CHADEMA, Lissu apita Makamu Mwenyekiti


Freema Mbowe amefanikiwa kutetea nafasi ya Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasi na Maendeleo (CHADEMA) Taifa kwa kupata ushindi wa asilimia 93.5.

Mbowe aliyepata kura 886 amemshinda Cecil Mwambe aliyepata kura 59 pekee sawa na asilimia 6.2 huku kura 3 zikitajwa kuharibika.

Tundu Lissu ameshinda nafasi ya Makamu Mwenyekiti Taifa (Bara) baada ya kupata kura 930 sawa na 98.8% akimshinda Sophia Mwakagenda (aliyetangaza kujitoa akiwa ukumbini) aliyepata kura 11 sawa na 1.2%.

Said Issa Mohamedi ameshinda nafasi ya Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa (Zanzibar) nafasi ambayo ilikuwa na mgombea mmoja.

Matokeo yote ya uchaguzi CHADEMA ni kama yanavyoonyesha chini.

MWENYEKITI WA TAIFA
1.Freeman Mbowe-886-93.5✔
2.Cecil David Mwambe- 59
3.HARIBIKA -3

MAKAMU MWENYEKITI BARA
1.Tundu Antipas Lissu-930-98.8%✔
2.Sophia H.Mwakagenda-11- 1..2%
HARIBIKA 9


MAKAMU MWENYEKITI ZANZIBARI
SAID ISSA MOHAMED
NDIYO 859-88.7%✔
HAPANA 95
HARIBIKA 1



No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...