Search This Blog
Sunday, December 15, 2019
Billbord Kutumia YouTube Kupanga Chati za Albamu
Sasa Idadi ya watazamaji ambao msanii anawapata kwenye mtandao wa Youtube itamsaidia kuingia kwenye chart za album za Billboard, Waandaji wa Chart hizo kubwa duniani wametangaza kuanza kujumuisha data za mtandao wa Youtube kwenye kupanga orodha ya charts.
Kuanzia Januari 3, 2020 Data za Audio na Video za Youtube na Mitindao mingine zitaanza kutumia kwenye kupanga chart kubwa zaidi za Album 'Billboard 200' Pia data za Apple, Spotify, Tidal na Vevo zitajumuishwa kwenye mahesabu yanayozipanga album 200 bora.
Data za video zimetangazwa kuongezwa ikiwa imepita miaka 5 tangu walivyotangaza kuanza kutumia pia data za Audio kwenye kupanga chart hizo ikiwa inahashilia mabadiliko ya chart hizo kutoka kwenye mpango wa kuzingatia viwango vya mauzo (sales) hadi kuanza kuzingatia mfumo wa utumiaji (consumption model).
Data za Youtube tayari zilikuwa zinatumiwa kwenye kupanga chart za nyimbo 'Billboard Hot 100' lakini hii inakuwa mara ya kwanza kuanza kutumiwa kwenye kupanga chart za album.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Punguza kilo tano kwa siku saba
NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...
-
Kiwanja kinauzwa kipo Dodoma Mahungu njia ya kwenda Singida kabala hujafika NALA. Kiwanja ni cha Makazi kinaukubwa wa Sqm 450 ( 15 X...
-
Akionekana kwa mara ya kwanza kwa umma tangu aondoke madarakani, aliyekuwa Rais wa Marekani Donald Trump ameweka wazi uwezekano wa kuwania...

No comments:
Post a Comment