Search This Blog

Sunday, December 29, 2019

Ajali ya Coaster na lori Yaua Watu 6 Dodoma

Watu sita wamefariki Dunia na wengine zaidi ya kumi kujeruhiwa katika ajali iliyohusisha gari aina ya Toyota Coaster na lori eneo la Kisasa Dodoma usiku wa kuamkia leo Dec 30,2019, Mganga Mfawidhi Hospitali ya Rufaa Dodoma Dr.Ernest Ibenzi amethibitisha kupokea miili ya Watu sita.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma, Gilles Muroto amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo na kusema kwamba chanzo chake ni dereva wa lori baada ya kuona korongo kubwa katikati ya barabara, akajaribu kulikwepa.

Amesema wakati anahama kukwepa korongo hilo, tayari lile basi dogo la abiria lilikuwa limeshafika karibu, na bodi la lori likaliangukia basi hilo la abiria na kusababisha vifo na majeruhi.Dereva alikimbia, Polisi wanaendelea kumsaka


No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...