
KLABU ya AC Milan inayoshiriki Ligi Kuu Italia imeongeza nguvu ya kutaka kumsajili mshambuliaji Zlatan Ibrahimovic aliyewahi kuichezea Inter Milan ya nchini humo.
Mshambuliaji huyo ambaye amemaliza mkataba wake na LA Galaxy, inaelezwa kwamba alikuwa kwenye mazungumzo marefu na Ac Milan lakini hawajaweza kumalizana.
Mabosi wa Milan wameamua kumuwekea ofa fupi ya mkataba wa miezi sita mpaka mwishoni mwa msimu ili kuangalia kama anaweza kukubaliana nao.
Vigogo hao wamejipanga kumpa ofa ya miezi sita kuanzia Januari huku kukiwa na kipengele cha kuongeza miezi 12 kwa mwaka ujao.
Zlatan amecheza klabu nyingi kubwa kwa miaka tofauti ikiwemo PSG, Manchester United na LA Galaxy.
No comments:
Post a Comment