TIMU ya Yanga imepokea kitita cha tsh milioni 10 kutoka kwa wadhamini wao, kampuni ya GSM ikiwa ni sehemu ya kuwapa motisha baada ya kuifunga Ndanda FC kwa bao 1-0 katika Uwanja wa Nangwanda Sijaona, jana Ijumaa, Novemba 8, 2019.
Patrick Sibomana ndiye aliibuka shujaa kwa kufunga bao moja la ushindi kwa Yanga dhidi ya Ndanda kwenye mchezo wa Ligi Kuu huku Yanga ikiwa chini ya Kaimu Kocha Mkuu, Boniface Mkwasa na msaidizi wake Said Maulid baada ya kumtimua Mwinyio Zahera.
Yanga iliwalazimu wasubiri mpaka dakika ya 75 kushinda mchezo huo mara baada ya Sibomana kupachika bao hilo kwa mpira wa adhabu akiwa nje kidogo ya 18 ambao ulizama jumla ndani ya nyavu za lango la Ndanda FC.
Ushindi huo unaifanya Yanga kufikisha jumla ya pointi 10 ikiwa imecheza mechi tano imeshinda mbili na imetoa sare tatu na kupoteza mchezo mmoja mbele ya Ruvu Shooting.
Kabla ya Mechi hiyo, GSM ilitoa ahadi ya kuipa Yanga Tsh milioni 10 endapo itashinda mechi hiyo na Wanakuchere, jambo ambalo Yanga wametekeleza hiyo kukabidhiwa zawadi hiyo.
Search This Blog
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Punguza kilo tano kwa siku saba
NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...
-
Kiwanja kinauzwa kipo Dodoma Mahungu njia ya kwenda Singida kabala hujafika NALA. Kiwanja ni cha Makazi kinaukubwa wa Sqm 450 ( 15 X...
-
Akionekana kwa mara ya kwanza kwa umma tangu aondoke madarakani, aliyekuwa Rais wa Marekani Donald Trump ameweka wazi uwezekano wa kuwania...

No comments:
Post a Comment