Search This Blog

Tuesday, November 26, 2019

Wakimbizi zaidi ya 100 wahamishwa kutoka Libya kwenda Rwanda



Kamishna Mkuu wa Shirika la kuhudumia wakimbizi la Umoja wa Mataifa (UNHCR) amesema shirika hilo limewahamisha wakimbizi zaidi ya 100 kutoka Libya kwenda Rwanda.

Taarifa iliyotolewa na shirika hilo imesema wakimbizi hao walioko hatarini wakiwemo watoto waliozaliwa katika vituo vya hifadhi nchini Libya, wamefika nchini Rwanda chini ya msaada wa kibinadamu ulioandaliwa na UNHCR.

Mjumbe maalum wa UNHCR kwa eneo la katikati la Mediterranean Bw. Vincent Cochetel amesema kutokana na ongezeko la vurugu mjini Tripoli, kuna uharaka wa kuhamisha maelfu ya wakimbizi, na kazi ya kuwasaidia kuondoka Libya ni ya dharura.

Pia ameushukuru Umoja wa Ulaya kwa kutoa dola za kimarekani milioni 10 kwa Utaratibu wa usafirishaji wa dharura (ETM) nchini Rwanda, ili kuwahamisha wakimbizi wengi zaidi kutoka Libya

No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...