Search This Blog
Monday, November 18, 2019
Serikali yalifunga Kanisa la Mfalme Zumaridi Jijini Mwanza
Uongozi wa Wilaya ya Nyamagana Mkoani Mwanza umepiga marufuku ibada zinazoendeshwa na kiongozi wa kanisa la Mfalme Zumaridi lililoko mtaa wa Iseni kata ya Butimba hadi hapo Serikali itakapojiridhisha kuwa ibada hazikinzani na sheria za nchi.
Agizo la kupiga marufuku limetolewa jana Novemba 18, 2019 na Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana Mkoani Mwanza Daktari Philis Nyimbi akiwa ameongozana na kamati ya ulinzi na usalama ya wilaya hiyo katika eneo la kanisa hilo.
Amesema kanisa hilo limekuwa likitumia katiba ya kanisa lingine ambalo ni Pentecoste Christian Church of Tanzania na pia limekuwa likitembea na Katiba ya Kanisa hilo.
DC Nyimbi amesema kiongozi wa Kanisa hilo la Mfalme Zumarid amekuwa akiendesha kanisa hilo bila kufuata sheria za nchi wala maandiko matakatifu kwa kujiita Mungu wa Dunia, Mfalme wakati yeye ni Mwanamke.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Punguza kilo tano kwa siku saba
NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...
-
Kiwanja kinauzwa kipo Dodoma Mahungu njia ya kwenda Singida kabala hujafika NALA. Kiwanja ni cha Makazi kinaukubwa wa Sqm 450 ( 15 X...
-
Akionekana kwa mara ya kwanza kwa umma tangu aondoke madarakani, aliyekuwa Rais wa Marekani Donald Trump ameweka wazi uwezekano wa kuwania...

No comments:
Post a Comment