Search This Blog

Saturday, November 9, 2019

Rosa Ree "Naombeni Mnisamehe"


MWANAMUZIKI wa kike wa Hipo Hop Bongo, Rosa Ree na ambaye inasemekana na mpenzi wa msanii wa Kenya, Timmy Tdat amewaomba msamaha mashabiki wake kufuatia kusambaa kwa video chafu ya wimbo alioutoa wiki iliyopita.  Rose Ree ameomba msamaha kwa Serikali ya Tanzania kwa kosa la kuonesha sehemu zake nyeti kwenye video hiyo ambayo ilikosolewa na maelfu ya mashabiki wake.

Rosa Ree aliliambia Gazeti la Ijumaa kuwa, anajutia kwa kitendo hicho kwani anaelewa vema kanuni za sanaa na kwamba siyo maadili ya Kitanzania. Alisema alikutana na na wakurugenzi wa bodi inayodhibiti filamu nchini na kuahidi kutorudia kosa kama hilo.

“Naombeni mnisamehe, naomba radhi kwa waliokwazwa na ile video iliyosambaa mtandaoni. “Nimefurahi kukutana na Bodi ya Filamu Tanzania na wamenielimisha mengi kuhusiana na sanaa na kanuni zake. “Tutaendelea kufanya kazi pamoja ili kuweza kuifikisha sanaa ya Tanzania mbali zaidi,” alisema Rosa Ree.

Stori: Imelda Mtema, Dar

No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...