Search This Blog

Friday, November 29, 2019

PSG kuwaleta pamoja Griezmann, Simeone

PARIS, UFARANSA . MIAMBA ya soka ya Ufaransa, Paris Saint-Germain imeripotiwa kwamba inataka kuwaleta tena pamoja kocha Diego Simeone na straika wake Antoine Griezmann kwenye kikosi hicho baada ya kutaka kuwanasa wote wawili kwa pamoja.
Kocha Thomas Tuchel bado anashikilia mikoba ya kuinoa PSG, lakini mabosi wa timu hiyo bado hawanna furaha kwa namna timu ilivyotupwa na Manchester United kwenye Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu uliopita.
Kwa mujibu wa taarifa za kutoka Ufaransa. PSG wanamtazama kocha wa sasa wa Atletico Madrid, Simeone kuwa ndiye atakayewafaa zaidi kwenye kuiongoza timu yao msimu ujao, huku mabingwa hao wa Ufaransa wakipiga hesabu pia za kumsajili staa wa Barcelona, Griezmann.
Griezmann aliachana na Atletico na kujiunga na Barcelona kwenye dirisha lililopita la majira ya kiangazi, lakini maisha yake huko Nou Camp yamekuwa magumu huku akidaiwa kwamba amekuwa hana uhusiano mzuri na supastaa wa kikosi hicho, Lionel Messi.
Wamiliki wa PSG wameliona hilo na sasa wanafikiria kuwaleta pamoja kwa mara nyingine wawili hao ili wakapige kazi kwenye kikosi chao wakiamini kwamba Barca watakuwa tayari kumpiga bei Griezmann mwishoni mwa msimu. Simeone amekuwa kwenye kiti cha kuinoa Atletico tangu Desemba 2011, akiiongoza kwenye mechi 448 za michuano yote.

Let's block ads! (Why?)

No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...