Search This Blog
Wednesday, November 13, 2019
Mtwara: Kijiji Chavamiwa, Watu Sita Wauawa kwa Risasi
Watu sita wameuawa katika kijiji cha Ngongo Wilaya ya Tandahimba mkoani Mtwara na wengine saba kujeruhiwa katika mpaka wa Tanzania na Msumbiji baada ya kuvamiwa na watu wasiojulikana usiku wa kuamkia juzi Jumanne Novemba 12, 2019.
Mkurugenzi wa Makosa ya Jinai (DCI), Robert Boaz amesema Watanzania sita walipigwa risasi na watu wanaodhaniwa kutoka nchi jirani ya Msumbiji wakati wakiwa visiwa vya mto Ruvuma wanakofanya shughuli za kilimo.
“Vyombo vya ulinzi na usalama vitahakikisha wahalifu hao wanapatikana na sheria kali zitachukuliwa juu yao, niwasihi tu wananchi kuepuka kwenda nchi za watu bila kuwa na vibali,” amesema.
Kwa upande wake Kamishna wa Operesheni na Mafunzo wa jeshi hilo, Leberatus Sabas, amesema kutokana na kazi nzuri wanayoifanya ndio maana wahalifu wanafanya matukio hayo mipakani.
“Tusikubali hata siku moja wavuke mpaka waje huku ndani tupo bega kwa mbega na wananchi. Vyombo vyote vya ulinzi na usalama vipo pamoja tutawasaka, tutawatia mbaroni na hatua kali zitachukuliwa.”
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Punguza kilo tano kwa siku saba
NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...
-
Kiwanja kinauzwa kipo Dodoma Mahungu njia ya kwenda Singida kabala hujafika NALA. Kiwanja ni cha Makazi kinaukubwa wa Sqm 450 ( 15 X...
-
Akionekana kwa mara ya kwanza kwa umma tangu aondoke madarakani, aliyekuwa Rais wa Marekani Donald Trump ameweka wazi uwezekano wa kuwania...

No comments:
Post a Comment