Search This Blog
Sunday, November 3, 2019
Mpenzi Mpya wa Vanessa MDEE Aanza Kuposti Mashemeji
Muigizaji maarufu duniani na star katika tamthilia ya power Rotimi ambaye kwa sasa kumekuwa na tetesii za kutoka kimapenzi na Vanessa mdee, ameposti mdogowake vanessa kupitia ukurasa wake wa instagram na kuandika kuwa Mimi Mars (am proud of you) najivunia wewe ni baada ya mwanamuziki huyo kutajwa katika tuzo za kalasha Awards.
Mimi mars ambaye kwa sasa yupo chini ya lebal ya mdee music, tarehe 30 alikuwa akifanya uzinduzi ya filamu ya You again aliyoshiriki na iliyooneshwa kwa mara ya kwanza Tanzania.
Mwanamuziki huyo na muigizaji, amechaguliwa kuwania tuzo ya Kalasha awards katika kipengele cha Best Acterss katika filamu aliyoigiza na waigizaji kutoka nchini Kenya inayoenda kwa jina la You Again.
Mimi mars ambaye aliwahi kuwa mtangazji na kuhamia katika tasnia ya muziki kwa sasa amijiingiza katika uigizaji huku akifanya vizuri na kuchaguliwa kuwania tuzo ambayo itamtambulisha vyema katika tasnia ya uigizaji.
Aidha mimi mars ametoa shukurani kwa wote waliojitokeza katika uzinduzi wa movie yake iliyooneshwa katika ukumbi wa Mlimani City Dar es Salaam.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Punguza kilo tano kwa siku saba
NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...
-
Kiwanja kinauzwa kipo Dodoma Mahungu njia ya kwenda Singida kabala hujafika NALA. Kiwanja ni cha Makazi kinaukubwa wa Sqm 450 ( 15 X...
-
Akionekana kwa mara ya kwanza kwa umma tangu aondoke madarakani, aliyekuwa Rais wa Marekani Donald Trump ameweka wazi uwezekano wa kuwania...

No comments:
Post a Comment