Search This Blog
Monday, November 11, 2019
Mahakama Tanzania yapanga kutoa maelekezo TLS kujiunga kesi ya Urais
Mahakama Kuu ya Tanzania imepanga kutoa maelekezo muhimu kuhusu maombi ya Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS) kujitosa katika kesi ya kikatiba inayohusu ukomo wa urais nchini humo, iliyofunguliwa na Mkulima, Patrick Dezydelius Mgoya.
TLS kimefungua maombi Mahakama Kuu kikiomba kuunganishwa katika kesi hiyo, huku katika hati ya faragha ya maombi hayo kikieleza kuwa kinaomba kuunganishwa katika shauri hilo kama mdaiwa mwenyewe maslahi.
Maombi hayo yaliyosajiliwa rasmi mahakamani Novemba 5, 2019, yalitajwa kwa mara ya kwanza jana Jumatatu Novemba 11, 2019 huku Mgoya ambaye ni mjibu maombi wa kwanza ndiye pekee aliyefika mahakamani.
Mjibu maombi wa pili, Mwanasheria Mkuu wa Serikali kwa niaba ya Serikali hakuwepo mahakamani wala mwakilishi wake, jambo ambalo lilimfanya Jaji Benhajj Masoud anayesikiliza maombi hayo ahoji kama alipewa taarifa na nyaraka za maombi hayo.
Wakili wa TLS, Suzan Kawanga aliieleza mahakama kuwa walimpa taarifa na nyaraka za maombi hao, tangu Ijumaa iliyopita, Novemba 8, mwaka huu.
Baada ya majadiliano mafupi kati yake na Mkulima Mgoya, Jaji Masoud alimpa siku tatu kuwasilisha kiapo kinzani kama atakuwa na hoja za kupinga maombi hayo kabla au kesho Jumatano.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Punguza kilo tano kwa siku saba
NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...
-
Kiwanja kinauzwa kipo Dodoma Mahungu njia ya kwenda Singida kabala hujafika NALA. Kiwanja ni cha Makazi kinaukubwa wa Sqm 450 ( 15 X...
-
Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano anayeshughulikia Sekta ya Ujenzi, Arch. Elius Mwakalinga, akitoa maelekezo kwa Kai...

No comments:
Post a Comment